Wednesday, July 21, 2010
Nyota wa Bayern "Ribery" ahojiwa na polisi
Mchezaji nyota wa soka wa kimataifa wa timu ya Bayern Munich,Frank Ribery, alizuiliwa na maafisa wa polisi hapo jana na kuhojiwa , akishukiwa kushiriki katika kitendo cha ngono kwa malipo na kahaba mwenye umri mdogo.
Ribery na mwenzake Karim Benzema, walihojiwa kwa muda wa masaa kadhaa katika makao makuu ya polisi mjini Paris. Kesi hiyo ilijulikana hadharani mwaka huu baada ya msichana mmoja mwenye umri mdogo, kujitokeza na kusema kuwa wachezaji kadhaa wa timu ya taifa ya Ufaransa walimlipa kufanya naye kitendo cha ngono. Hatahivyo uchunguzi wa kesi hiyo uliahirishwa ili usiingiliane na matayarisho ya Ufaransa kushiriki katika mashindano ya kombe la dunia. Wakili wa Ribery amesema nyota huyo wa Bayern, hakujuwa kuwa msichana huyo ana umri wa chini ya miaka 18.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment