Mabingwa wa soka nchini Uingireza timu ya Chelsea, wametangaza kwamba mshambuliaji wao machachari Didier Drogba hatauzwa.
Timu hio ya Chelsea wametangaza hayo baada ya wakala wa mchezaji huyo Thierno Seydi kusema kwamba kuna uwezekano wa Drogba kuuzwa kwa timu ya Manchester City.
Wakala huyo alisikika katika kituo kimoja cha radio akisema kwamba Drogba ataondoka Chelsea kwenda City kabla ya kipindi cha uhamisho kumalizika, kitendio ambacho kimepelekea Chelsea kutoa tamko.
Timu ya Machester City ilimtaka Drogba kwa msimu ujao wa ligi lakini hadi sasa imeshindikana kwa mchezaji huyo kuondoka Stamford Bridge, katika msimu wa ligi uliomalizika Drogba mwenye umri wa miaka 32 aliweza kupachika mabao 29 katika ligi kuu nchini Uingereza.
No comments:
Post a Comment