Thursday, July 8, 2010

CHAMA CHA CCM KUTEUA WAGOMBEA WA URAIS

Wajumbe wa chama tawala nchini Tanzania, Chama cha Mapinduzi, CCM, wanakutana leo katika mji wa Dodama, kuwateuwa wagombea wa Urais wa Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania pamoja na wagombe wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar.

Kumekuwa na kampeini za usiku kucha huku wagombea wakiwashawishi wajumbe kuwaunga mkono. Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari nchini humo, watu watano wamejitokeza kuwania kiti cha Urais kisiwani Zanzibar.

Watano hao ni pamoja na waziri wa zamani Dr Mohamed Bilal, makamu wa rais Dr Ali Mohamed Shein, waziri kiongozi Shamsi Vuai Nahodha, na naibu wake Ali Juma Shamhuna na waziri wa elimu Amali Haroun Ali Suleiman.

Watano hao watakuwa wakiwania nafasi ya kumrithi rais Amani Karume ambaye muda wake wa kuhudumu kama rais unamalizika mwaka huu. Rais wa Jamuhuri ya Muungano Jakaya Kikwete, anatarajiwa kuidhinishwa tena kuwania kiti hicho kwa muhula wa pili.

Kufikia sasa hakuna mwanasiasa yeyote ambaye amejitokeza kumpiga rais Kikwete. Matokeo ya kongamano hilo yanatarajiwa kutolewa abaadaye hii leo.

***BBC

No comments:

Post a Comment