Tuesday, July 6, 2010
BAYERN MUNICH WACHANGANYIKIWA NA VAN DER WIEL
Mabingwa wa soka nchini Ujerumani Bayern Munich wametangaza jumla ya euro milioni 13 kwa kutaka kumnunua beki wa kulia wa timu ya Ajax Amsterdam ambae pia anaichezea timu ya taifa ya Holland (Oranje) Gregory van der Wiel.
Lakini hadi sasa timu ya Ayax haijathibitisha ikiwa imeshapokea ombi hilo kutoka kwa Bayern.
Awali timu ya Ayax ilitangaza kwa yoyote anaemtaka mchezaji huyo wataweza kumuuza si chini ya euro milioni 20, sasa haijajuilikana iwapo Bayern watafanikiwa ama azma yao itagonga ukuta.
Van der Wiel mwenye umri wa miaka 22 ambae ndio chaguo namba moja kwa kocha wa Oranje Van Marwijk ameonesha kiwango cha hali ya juu katika mashindano ya kombe la Dunia yanayoendelea huko Afrika Kusini amekua akiendewa mbio pia na timu kubwa kama vile Manchester City,Arsenal, Real Madrid, Barcelona na Juventus.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment