Monday, June 7, 2010

WASHUKIWA WA UGAIDI WAKAMATWA NEWYORK

Polisi jijini New York nchini Marekani wamewakamata wanaume wawili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa John F. Kennedy, ikiwa ni sehemu ya upelelezi, ambapo vyombo vya habari vimearifu kuwa wanahusishwa na mtandao wa al Qaida.

Gazeti moja nchini Marekani limearifu kuwa watu hao walikuwa wanapanga kwenda Somalia kujiunga na kundi la waislam wenye msimamo mkali. Watu hao walikuwa wapande ndege tofauti kuelekea Misri.

Inaarifiwa kuwa nyumba za watuhumiwa hao pia zilifanyiwa upekuzi na maafisa wa idara ya upelelezi ya Marekani FBI. Watu hao leo wanatarajiwa kupandishwa kizimbani katika mahakama ya New Jersey, kukabiliana na makosa ya kujihusisha na vitendo vya ugaidi.

Kukamatwa kwao kunafuatia jaribio lililoshindwa la kutaka kuripua eneo maarufu la Times Square kwa bomu lililotegwa kwenye gari mwezi uliopita.

No comments:

Post a Comment