Thursday, June 10, 2010

VYAMA VYA UPINZANI VYAIBUKA NA USHINDI NCHINI UHOLANZI

Matokeo ya uchaguzi wa bunge nchini Uholanzi hayakutoa ushindi kamili kwa chama chochote lakini yanaonyesha kuwa wapigakura nchini humo wameamua kubadilisha serikali.

Chama cha Christian Democratic Action cha waziri mkuu anayeondoka madarakani Jan Peter Balkenende kimepata pigo katika uchaguzi huo, kikipoteza nusu ya viti vyake bungeni. Kutokana na hali hiyo, Balkenende ametangaza kujiuzulu kama kiongozi wa chama hicho, na kuacha kiti chake bungeni.

Chama cha mrengo wa kati kulia cha Kiliberali na kile cha mrengo wa shoto kati cha Labour vimefungana kwa kupata viti 31 kila kimoja kutoka viti 150, wakati chama kinachopinga wahamiaji kimekuwa cha tatu kwa kupata viti 22.

Chama cha Christian Democratic kimeshika nafasi ya nne. Chama cha Kiliberali kilitarajiwa kushinda kutokana na uchunguzi wa maoni ya wapiga kura kabla ya uchaguzi.

No comments:

Post a Comment