Monday, June 21, 2010

TIMU YA UFARANSA YAGOMEA MAZOEZI

Timu ya Ufaransa imegomea mazoezi, ikiwa ni kupinga hatua ya kurejeshwa nyumba kwa mshambuliaji nyota wa timu hiyo Nicolas Anelka.

Anelka alitimuliwa kutoka katika timu hiyo baada ya kumtolea lugha chafu kocha wake wakati wa mapumziko kwenye mechi kati yao na Mexico ambapo walifungwa mabao 2-0.

Mgomo huo umesababisha mkurugenzi wa timu hiyo ya Ufaransa Jean-Louis Valentin kujiuzulu.Ufaransa inawajibika kushinda mechi yao ya mwisho dhidi ya Afrika Kusini, na wakati huo ikitegemea, matokeo katika mechi kati ya Uruguay na Mexico, ili kufuzu kwa raundi ya pili.

Taarifa za kutokea kwa kadhia hiyo ziliripotiwa katika vyombo vya habari vya Ufaransa ambapo Rais wa nchi hiyo Nicolas Sarkozy amekosoa tabia ya Anelka pindi itakua ni kweli.

Wakati huo huo, Brazil jana ilikuwa timu ya pili kufuzu kwa duru ijayo baada ya kuifunga Ivory Coast mabao 3-1.

Muda mfupi ujayo Ureno itapambana na Korea Kaskazini, kabla ya Chile kucheza na Uswis na baadaye Uhispania itajaribu kufufua matumaini yake mbele ya Honduras

No comments:

Post a Comment