Thursday, May 6, 2010

RAIS UMARU YAR 'ADUA WA NIGERIA AFARIKI DUNIA


Rais Umaru Yar'Adua wa Nigeria wa amefariki.

Rais huyo alikuwa mgonjwa sana kwa muda mrefu na alishindwa kutokea hadharani.

kutokana na hali mbaya ya afya alipelekwa Saudi Arabia mwezi Novemba mwaka jana kwa ajili ya matibabu ya maradhi ya moyo na figo.

Hata hiyvo hali yake haikuwa nzuri na alirejeshwa Nigeria mnamo mwezi Februari na tokea wakati huo hakutokea tena hadharani.

Bunge la Nigeria lilipitisha azimio mnamo mwezi huo huo wa Februari ili kumkabidhi mamlaka makamu wake Dr. Goodluck Jonathan ya kuwa kaimu rais.

Msemaji wa rais amewaambia waandishi habari kwamba Yar'Adua atazikwa leo katika jimbo lake la uzawa la Katsina kaskazini mwa Nigeria.

Rais Yar'Aradua alikuwa na umri wa miaka 59.

Kifo chake kitaombolezwa kitaifa kwa muda wa siku saba.


.

No comments:

Post a Comment