Wednesday, May 5, 2010

MWANAMKE APIGWA FAINI KWA SABABU YA KUVAA NIQAB HADHARANI


Mwanamke mmoja mwenye asili ya Tunisia amehukumiwa adhabu ya kulipa faini ya Euro mia tano kwa sababu ya kuvaa hadharani vazi linalofunika uso na kuacha macho tu, Nikab.

Mama huyo mwenye umri wa miaka 26 alisimamishwa na polisi katika mji wa Novara kaskazini mwa Italia wakati akiwa njiani kuelekea msikitini.

Alipewa adhabu hiyo kwa mujibu wa sheria za mji huo.

Nako nchini Ujerumani waziri wa mambo ya ndani Thomas de Maiziere amesema mjalada juu ya kupiga marufuku mavazi yanayofunika mwili mzima Burka, au uso tu,Nikab, haufai na siyo lazima.



.

No comments:

Post a Comment