Wednesday, May 5, 2010

EURO YAANGUKA DHIDI YA DOLA

Masoko ya dunia yamepiga mbizi kutokana na wasiwasi wa waweka vitega uchumi juu ya uwezekano wa mgogoro wa madeni barani Ulaya kuwa mkubwa zaidi licha ya kupitishwa kwa mpango wa kuiokoa Ugiriki.

Sarafu ya Euro, ilianguka mbele ya dola, kwa kiwango ambacho hakijawahi kufikiwa mnamo mwaka huu.

Masoko muhimu ya hisa pia yalianguka kwa asilimia moja nukta nne.

Masoko muhimu ya hisa ya Uhispania na Ureno pia yalianguka kwa asilimia nne kutokana na wasiwasi wa waweka vitega uchumi wanaohofia kwamba huenda Ureno na Uhispania zikafuata mkumbo wa Ugiriki kwa kutumbukia katika mgogoro wa uchumi.


.

No comments:

Post a Comment