Tuesday, May 4, 2010

KWA MARA NYENGINE TENA SAFARI ZA NDEGE ZAPIGWA MARUFUKU KATIKA ANGA AYA IRELAND

Mara nyingine tena, Ireland imepiga marufuku safari za ndege nchini humo kwa sababu ya hatari inayosababishwa na wingu jipya la majivu ya volkano kutoka Iceland. Maafisa wanaosimamia misafara ya ndege nchini humo wamesema, ndege hazitoruhusiwa kutua au kuruka kutoka viwanja vya ndege vya Ireland, kuanzia saa mbili asubuhi za Ulaya ya Kati hadi nane mchana.

Maafisa hao wamesema, kiwango cha majivu ya volkano katika anga ya Ireland ni kikubwa mno.Baadhi ya misafara ya ndege imefutwa hata katika eneo la Scotland,kaskazini mwa Uingereza.

Lakini safari za ndege katika sehemu zingine za Uingereza na barani Ulaya hazikuathirika.

Mwezi uliopita wingu kubwa la majivu ya volkano lilisababisha safari zote za ndege kupigwa marufuku kwa siku sita katika nchi nyingi barani Ulaya.Takriban abiria milioni 3 walikwama kwenye viwanja vya ndege.

Leo mawaziri wa usafiri wa nchi za Umoja wa Ulaya wanakutana Brussels kushauriana kuhusu vurugu lililosababishwa wakati huo.

.

No comments:

Post a Comment