Saturday, April 24, 2010

UGIRIKI YAOMBA MSAADA KUTOKA ULAYA NA IMF

Serikali ya Ugiriki inayokabiliwa na kitisho cha kufilisika, imeomba msaada kutoka kwa washirika wenzake katika kanda inayotumia sarafu ya Euro na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF.

Waziri wa Fedha wa Ugiriki, George Papaconstantinou amesema msaada wa fedha kutoka nchi za kanda ya Euro na shirika la fedha la kimataifa , IMF upo njiani lakini utachukua siku kadhaa kabla ya kufika nchini humo.

Siku ya Ijumaa, Ugiriki ilitoa ombi kwa Umoja wa Ulaya na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF, kuipatia msaada wa Euro bilioni 45 ili iweze kulipa madeni yake makubwa.

Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel. amesema, kuna masharti ya kutimizwa. Kwanza, mpango unaoaminika kupunguza matumizi, ujadiliwe kati ya Ugiriki, Kamisheni ya Ulaya na Shirika la Fedha la Kimataifa. Pili, mpango huo utakapowasilishwa, basi Kamisheni ya Ulaya, Benki Kuu ya Umoja wa Ulaya na Shirika la Fedha la Kimataifa lazima zitathmini ikiwa hali ya sarafu ya Euro inalazimisha kuisaidia Ugiriki."

Baada ya kutimizwa kwa masharti hayo mawili, masuala mengine kuhusu kiwango na njia ya kutoa msaada huo yanaweza kujadiliwa.

.

No comments:

Post a Comment