Thursday, April 1, 2010

SEMENYA KWENDA MAHAKAMANI


Bingwa wa dunia wa mbio za mita 800 Caster Semenya, huenda akaenda mahakamani ikiwa atakataliwa kushiriki katika mashindano ya riadha kutokana na utata wa jinsia yake iwapo yeye ni mwanaume au mwanamke.

Gazeti la Star la Afrika Kusini limeripoti kuwa mawakili wa Semenya wataenda mahakamani Jumatatu endapo chama cha riadha nchini humo-ASA kitamzuia asikimbie katika mashindano yanayotarajiwa kufanyika wiki ijayo huko Germiston, Afrika Kusini.

Taarifa hizi zimetolewa siku moja baada ya msemaji wa ASA,
Richard Stander kusema kuwa Semanya hawezi kushiriki katika mashindano kabla jinsia yake haijajulikana na kutangazwa na Shirikisho la Riadha Ulimwenguni-IAAF. Semenya hajashiriki katika mashindano yoyote ya riadha tangu yalipofanyika mashindano ya mwaka 2009 mjini Berlin, ambapo IAAF ilitangaza kuwa inachunguza jinsia yake baada ya kushinda nishani ya dhahabu katika mbio za mita 800.

.

No comments:

Post a Comment