Friday, April 2, 2010

ROONEY KUKAA JUU KWA MUDA WA WIKI TATU


Mshambuliaji tegemeo wa timu ya Man U Wyne Rooney ambae aliumia kwa sasa anasumbuliwa na ankle sasa imethibitishwa kwamba atakaa juu kwa muda wa wiki tatu.

Rooney aliumia siku ya Jumatano wakati Man U walipocheza dhidi ya Baryen na kupelekea hofu kubwa kwa Waingereza na wapenzi wa Man u kwamba angeweza kukosa kucheza Kombe la Dunia.


Hofu hio iliondoka mara tu baada ya Rooney kufanyiwa Scanning na kugunulika kua hakuumia sana kama ilivyokua ikidhaniwa kabla.


Kwa upande wake kocha wa Man U, Sir Alex Ferguson amethibitisha ya kwamba Rooney atarejea uwanjani baada ya kipindi cha wiki tatu.

"Hakuumia sana kama ilivyokua ikidhaniwa mwanzo, na atarejea uwanjani baada ya wiki tatu.
"Mara nyingi huwa inahofiwa pale mchezaji anapofaniwa Scanning, lakini matokeo ni mazuri na hakuna mfupa ulioathirika.

"Kila mtu anataka wachezaji wake ambao ni tegemeo waweze kucheza, Taifa linaweza kupumua tena, tumefarijika, na hii ingelikua mbaya zaidi" amesema Ferguson.

Jeraha hili la Rooney linampeleka nje na kukosa mechi muhimu kama ile ya siku ya Jumamosi wakati Man U watakapocheza na Chelsea na pia mechi ya marudiano dhidi ya Baryern Jumatano ijayo, lakini anaweza kuonekana tena siku ya tarehe 17 mwezi ujao wakati Man U watakapo wakapokiminya na Derby.



.

No comments:

Post a Comment