Saturday, April 17, 2010

SAFARI ZA NDEGE ZIMEFMUTWA KATIKA NCHI NYINGI ZA ULAYA

Eneo kubwa la bara la Ulaya bado haliwezi kutumiwa kwa misafara ya ndege kwa sababu ya wingu kubwa la majivu lililosababishwa na mripuko wa volkano nchini Iceland.

Shirika linaloratibu safari za ndege barani Ulaya-Eurocontrol, limesema kuwa hii leo kiasi ya safari 16,000 za ndege zimefutwa kwa sababu ya wingu hilo la majivu.

Kenneth Thomas wa shirika hilo amesema wingu hilo linaendelea kusambaa.

Shirika la usalama wa anga la Ujerumani-DFS limesema anga ya Ujerumani itaendelea kufungwa hadi kesho saa nane usiku.

Maafisa wa misafara ya ndege wamesema, mashirika ya ndege yanapata hasara ya takriban euro milioni 150 kwa siku kwa sababu ya mvurugo wa safari za ndege.

Wataalamu wa volkano nchini Iceland wamesema, ionekanavyo volkano hiyo imepungua kufoka, lakini huenda ikaendelea kufoka kwa siku kadhaa zijazo au hata miezi ijayo.

.

No comments:

Post a Comment