Friday, April 9, 2010

MTOTO AJINYONGA JIKONI

Mtoto mwenye umri wa miaka 10 amejinyonga katika jiko la nyumbani kwao, Dar es Salaam.

Mtoto huyo, Aisha Zuberi, alikutwa amekufa jana saa moja usiku, Kigogo Kati katika wilaya ya Kinondoni.

Mtoto huyo aliyekuwa akisoma darasa la nne katika shule ya Barafu, ni miongoni mwa watu watano walioaga dunia katika matukio tofauti mkoani jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa kaka wa marehemu, Maneno Idd (38), kabla ya kujinyonga, Aisha alikuwa anachezea swichi ya umeme iliyoharibika, mama yake akamkataza.

“Inasemekana kuwa alipoonekana anachezea ile swichi ya umeme mama yake alimkanya asichezee na akaacha mara moja,” amesema Idd na akaongeza kuwa, baada ya muda wazazi wa mtoto huyo walitoka kwenda kumuona mgonjwa nyumba ya nne jirani.

“Na wakati wazazi wanatoka waliacha hela kwa mdogo wa marehemu aitwae Mahmoud kwa ajili ya kununua sambusa,” amesema Idd.

Idd alisema kwamba baada ya kula sambusa, marehemu aliwaacha wenzake nje, akaenda ndani, akajifungia jikoni.

Kwa mujibu wa Idd, baada ya mama wa mtoto huyo kurudi, alikwenda jikoni ili awashe jiko apike, akakuta mlango umefungwa.

Idd amesema, baada ya mlango huo kufunguliwa walimkuta Aisha amejinyonga dirishani akiwa amekaa katika kiti.

Inadaiwa kwamba, marehemu hakuacha ujumbe wowote hivyo chanzo cha kifo hicho hakijulikani.


.

1 comment:

  1. Huu nimsiba mkubwa lakini hawa wazazi wa marehemu hawajasema ukweli mambo yamefichika inawezekana marehemu kapigwa sana kwa sababu alikatazwa kuchezea switch lakini utoto hakusikia ndipo akapigwa sana na marehemu kaamua kujitowa roho, au kaivunja switch ya umeme akaogopa mama akirudi atapewa adhabu kali akaona bora aondoka kabla ya mama kuja haya ni maoni

    ReplyDelete