Monday, April 5, 2010

MAHARAMIA WA KISOMALI WATEKA NYARA MELI YA KOREA KUSINI

Meli kubwa ya mafuta ya Singapore inayotumika na Korea Kusini kusafirishia mafuta imetekwa nyara na maharamia wa kisomali katika bahari Hindi siku ya Jumapili.

Meli hiyo yenye tani elfu miatatu ijulikanayo kama Samho Dream, ilitekwa ikiwa imebeba mafuta ghafi kuelekea Marekani kutoka nchini Iraq.

Mahabaria ishirini na wanne walikuwemo kwenye meli hiyo ambao raia 5 wa Korea ya Kusini na Wafilipino 19 wamezuiliwa mateka.

Korea kusini tayari imepeleka manowari yake ya kijeshi takriban kilomita elfu moja miatano kusini mashariki mwa Ghuba ya Aden, ambako inaaminika meli hiyo imetekwa, kuizuia kuelekezwa katika bandari yoyote.

Maharamia waliolenga kuteka meli katika fuo za Somalia mwaka jana, walijitajirisha kwa kulipwa mamilioni ya dola kama kikombozi.


.

No comments:

Post a Comment