Friday, April 30, 2010

LEO NI SIKU YA KUZALIWA MALIKIA BEATRIX WA NEDERLANDS




Mnamo tarehe 31, 1938 at Palies Soestdijk Princess Beatrix wa Nederlands alizaliwa, na yeye ndio mtoto wa mwanzo katika familia ya prencess Juliana and Prince Bernhard.

Jina lake kamili anaitwa Beatrix Wilhelmina Armgard of Orange-Nassau, na wazazi wake waliamua kumpa jina la Beatrix, ambalo maana yake halisi ni Furaha.

Prince Beatrix baadae alipata ndugu watatu ambao ni pamoja na Irene ambae alizaliwa mwaka 1939, Margriet aliyezaliwa mwaka 1943 na Mary aliyezaliwa 1947).

Miaka miwili na nusu baada ya Beatrix kuzaliwa Wajerumani walivamia Nederlands pamoja na Belgium mnamo tarehe 10 may 1940 katika vita vikuu vya pili vya Dunia, ambapo Beatrix na ndugu zake walikimbizwa na kupelekwa Canada ambako walipewa hifadhi kutokana na vita hivyo vya pili vya Dunia, na huko Canada ndiko ndugu yake wa pili Margriet alikozaliwa kwenye mwaka 1943, na baadae walirejea Nederlands katika kijiji cha Palies soestdijk mjini Baarn.

Mnamo mwaka 1956 baada ya kumaliza masomo yake ya sekondari Beatrix alihama Baarn na kuhamia Leiden, ambako aliendelea na masomo ya chuo kikuu katika fani ya sociology na history,

Licha ya uchunguzi uliofanywa na Serikali kuhusu mchumba wa Beatrix ambae ni Mjerumani aliyetuhumiwa kuwa mfuasi wa Hitler,mnamo tarehe 10 machi 1966 Beatrix na Claus walifunga ndoa huko Amsterdam, ambapo watu walianadamana na kupiga mabomu kwa kupinga ndoa hio.

Licha ya migongano iliyotokea kati ya Wanederands na Claus, baadae Wanederlands walikubaliana na hali halisi na hatimae walimkubali Claus, na hatimae wawili hao walifanikiwa kupata watoto watatu, Willem-Alexander ambae alizaliwa mwaka 1967, Johan Friso aliyezaliwa mwaka 1968 na Constantine aliyezaliwa mwaka 1969.

Mnamo tarehe 30 April 1980 Beatrix alitawazwa rasmin kuwa mtawala wa Nederlands, na katika sherehe za uzinduzi zilizofanyika Dam huko Amsterdam kulitokezea mapigano ya wananchi kufuatia hali mbaya ya uchumi iliyokua ikiikabili Nederlands kwa wakati huo lakini polisi walifanikiwa kuwatawanya waandamanaji na watu wengi walilazwa spitali.

Mnamo mwaka 1981 Beatrix alihamia Den Haag (The Hague) yeye na familia yake kwenye Palace ya Huise ten Bosh ambayo iko mjini Den Haag, ambapo baadae alifanikiwa kuuuinua uchumi wa Nederlands.

Kutokana na afya ya Prince Claus kudhoofika kutokana na ugonjwa aliokua nao wa kensa mnamo tarehe 6 Octoba 2002 alifariki dunia katika spitali ya Academic Medical Centre huko Amsterdam, na katika mwaka 2004 wazazi wote wawili wa Beatrix walifariki dunia.

.

No comments:

Post a Comment