Monday, April 19, 2010

HISPANIA YAITISHA MKUTANO WA MAWAZIRI WA USAFIRI

Safari za anga katika bara la Ulaya bado zinaendelea kusitishwa, wakati wingu la majivu ya volcano kutoka nchini Iceland likiendelea kuathiri bara hilo.

Kwa muda mfupi jana Jumapili, safari chache zilifanyika katika viwanja vya ndege nchini Ujerumani, lakini hivi sasa safari zote nchini humo zitaendelea kusitishwa hadi saa nane mchana saa za Ulaya ya kati leo Jumatatu.

Kiasi cha nchi 30 zimefunga ama kuzuwia anga zao kutokana na hofu ya usalama wa abiria, na kuzuwia karibu wasafiri milioni saba ambao hawakuweza kusafiri duniani kote.

Hispania ambayo ni rais wa umoja wa Ulaya kwa sasa , imeitisha mkutano utakaofanyika kwa njia ya simu ya video kwa ajili ya mawaziri wa usafirishaji wa umoja wa Ulaya leo Jumatatu kutathmini hali hiyo.

Hapo mapema waziri wa Hispania anayehusika na masuala ya umoja huo amesema kuwa inawezekana kuwa nusu ya safari za anga kufanyakazi leo Jumatatu.

.

No comments:

Post a Comment