Thursday, April 1, 2010

BURQA KUPIGWA MARUFUKU UBELGIJI
Kamati ya Bunge la Ugelgiji inayohusika na masuala ya ndani ya nchi, imepiga kura kupiga marufuku kuvaa hadharani vazi la kiislamu la kujifunika kuanzia uso hadi miguu, aina ya buibui, maarufu kama Burqa .

Wajumbe wa kamati kwa pamoja walipiga kura kupiga marufuku vazi lolote la nguo au buibui linalomzuwia mtu kutambuliwa, ikiwemo Hijab inayoziba uso mzima.


Hatua hiyo ambayo inatarajiwa kupitishwa kirahisi na bunge, inatoa njia ya kuweza kuanza utekelezaji wa sheria hiyo nchini Ubeligiji na kuwa ya kwanza barani Ulaya.


Burqa ni aina ya vazi ambalo huvaliwa na wanawake wa kiislamu nalo hufunika mwili wote na katika sehemu ya macho huwekwa kitambaa chepesi aina ya nyavu nyavu ambayo humuwezeka mtu kuona ila yeye hawezi kuonekana hata macho yake.

Vazi hili la Burqa linafanana sana na vazi la Niqab ila kwa upande wa vazi la niqab hufunika mwili wote na kubakisha sehemu ya macho tu ambayo humuwezesha mtu kuona na yeye pia huweza kuonekana sehemu hio ya macho.

Nchi kadhaa barani Ulaya zimeonesha nia yao ya kuyapiga marufuku mavazi haya mawili huku nchi nyengine zikiwa na lengo la kupiga marufuku vazi zima linalohusiana na Hijab.

Ama kwa upande wa vazi la Hijab, vazi hili hua ni aina ya kitambaa kinachofunika nywele pamoja na shingo na kuwacha sehemu ya uso ikiwa wazi, na kitambaa hichi kuwa ni cha pembe tatu ingawa watu huchukulia kwamba kila kitambaa kinachovaliwa na wanawake wa kiislamu kichwani ni Hijab.

Licha ya kuwa vazi hili linachukuliwa ni kwamba ni vazi la kiislamu lakini kwa ujumla vazi hili linaashiria ujanajike zaidi, na hii ni kwa sababu kuna watu wengi ambao sio waislamu nao hupenda kulivaa vazi hili.
.

No comments:

Post a Comment