Wednesday, March 17, 2010

WAPALESTINA KADHAA WAJERUHIWA JERUSALEM

Mapambano yaliyotokea jana kati ya Wapalestina na Jeshi la Israel, katika mji wa Jerusalem yamesababisha Wapalestina wapatao 100 kujeruhiwa.

Serikali ya Israel nayo imearifu kuwa wanajeshi wake wapatao 14 pia walijeruhiwa katika ghasia hizo.

Ghasia hizo zilisababishwa na kufunguliwa na hekalu la kiyahudi katika maeneo matakatifu ya waislamu mashariki mwa Jerusalem.

Wakati hayo yakitokea kiongozi wa ngazi za juu wa Hamas ametoa wito wa kufanya maasi mapya ama intifada.

Katika siku za hivi karibuni, uamuzi wenye utata wa Israel wa kujenga nyumba mpya elfu moja na 600, kwa ajili ya makaazi ya wayahudi, mashariki mwa Jerusalem umeathiri pia uhusiano kati ya Israel na Palestina.

Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya, Ujerumani na Marekani pia zimekosoa hatua hiyo ya Israel.

Aidha jana maafisa wa Israel walitangaza kuwa mjumbe maalumu wa Marekani mashariki ya kati George Mitchell ameahirisha mpango wake wa kufanya ziara katika eneo hilo.


.

No comments:

Post a Comment