Wednesday, March 17, 2010

MOURINHO: SHUJAA WA STAMFORD BRIDGEAlikua ni kocha wa timu ya Chelsea ya Uingereza lakini akaja kufukuzwa na bosi wa timu hio Roma Abramovic ktika Mwaka 2007 licha ya kuipatia Chelsea zawadi tano, nae si mwengine ni Jose Mourinho.

Jana ilikua ni mara ya pili kwa Mourinho akiwa na timu ya Inter kukutana na timu yake hio ya zamani kwa mwaka huu katika mashindano ya Champions League. ambapo jana Inter ilishinda goli moja lililofungwa na Eto'o.

Mara ya kwanza walikutana katika uwanja wa Stadio Giuseppe Meazza, kabla ya mechi hio ya kwanza Mourinho alijigamba sana kwamba Chelsea ni vijana wake na hakuna sababu ya kutowafunga kwani anawajua juu chini, hatimae hata firimbi ya mwisho inalia Inter ikaibuka mshindi wa magoli 2-1.

Baada ya mechi ya jana alipofanya mahoniano alisema Timu yake imecheza viruzi na ndio maana imeshinda.

"Baadhi ya wakati katika mpira unaweza ukashinda kwa sababu una bahati, au kuna kitu kimetokea katika mchezo ambacho kimesababisha mpira kubaki sehemu moja ya uwanja na kutokwenda sehemu ya pili ya uwanja.

"Baadhi ya wakati unashinda kwa sababu wewe umecheza vizuri zaidi kuanzia dakika ya mwanzo hadi ya mwisho wa mchezo.

"Sasa timu hiyo ndio ilikua timu yangu, vijana wangu, wamenifurahisha sana wao pamoja na washabiki wa Inter, ambao wafika hadi muda huu bila ya kufika katika hatua ya robo fainali.

"Na nimefurahi nafsi yangu kwa kua nimefanya bidii na ili kufanikiwa hili", alisema Mourinho.

Katika mechi hio ya jana Mourinho hakuonekana kua na shangwe kama alivyozoeleka wakati Samuel Eto'o kuweka mpira kwenye nyavu kwenye dakika ya 78, lakini alikiri kua alifurahi sana walifofika dressing room.

"Nilisherehekea sana Dressing room, kama nitaakuja hapa tena, nitafundisha timu nyengine ya Kiengereza na nitakuja kama ni mpinzani kwa mara nyengine tena.

"Kama mtaalamu, hizi ni hisia bora zaidi unaweza kuwa nazo, sifurahii kwa sababu wachezaji wangu wa zamani au Roman wamepoteza, au washabiki wa Chelsea wamerudi nymbani na huzuni, sina furaha kutokana na huzuni waliyonayo.

"Lakini haya ndio maisha, jana nilizungumza na John Terry na nilimwambia kua mmoja kati yetu anaweza kua na huzuni leo, na haya ndio maisha".

.

No comments:

Post a Comment