Monday, March 8, 2010

PATO NA SEEDORF WAKO FITI KWA SAFARI YA OLD TRAFFORD


AC Milan inatarajiwa kuondoka Italy kesho kwa safari ya kuelekea katika jiji la Mchester tayari kwa mchezo wao dhidi ya Man United siku ya Jumaatano kwa kuwania kombe la Champions League, mshambuliaji wa Kibrasil Alexandre Pato amethibitishwa kuwa yuko fiti baada ya mazoezi ya leo asubuhi.


Pato alipata majeraha siku ya tarehe 28 Febuari, lakini anaonekana kupona kwa wakati muafaka, wakati ambapo AC Milan wana kibarua kigumu kwenye Champions League.


Kwa upande wa Clarence Seedorf ambae nae aliumia baada ya mchezo wao wa mwanzo walipocheza dhidi ya ManU kwa sasa yuko gado kwa ajili ya mtanange huo wa pili dhidi ya Manchester United, amethibitisha Kocha Leonardo.

No comments:

Post a Comment