Wednesday, March 3, 2010

FIFA/Coca-Cola WORLD RANKING


Shirikisho la soka ulimwenguni FIFA leo hii limetoa orodha ya kila nchi na nafasi yake inayoshikilia katika mchezo wa mpira Duniani ( World Ranking).


Katika orodha hio iliyotoka leo ambayo hutolewa kila mwezi imeonesha mabadiliko makubwa kwa baadhi ya nchi na kuzibakisha timu nne zinazoshikilia nafasi za mwanzo zikiwemo 1. brazil 2. Netherland 3 . Spain na 4. Italy bila ya kubadilika, huku mabingwa wa Soka barani afrika Egypt wakiwa kwenye nafasi ya 17 ikiwa imeshuka kwa nafasi 7 huku ikiwa imepotrza alama 102.


Timu itanashiriki mashindano ya World Cup 2010, ambao ndio wenyeji wa mashindano hayo South Africa, ndio timu pekee ambayo haimo kwenye African top 10, kwenye orodha hii inaonekana kuwepo kwenye nafasi ile ile ya 81 nafasi ambayo waliipata mwezi disemba 2009 walipotoka kwenye nafasi ya 85baada ya kupata 14 za ziada.


Watoto wa Maximo soka lao linaonekana kushuka kila siku licha ya usemi kwamba soka la bongo limekua, hii iko dhahir kwa sababu timu hii ya Tanzania ilikua kwenye nafasi ya 94 mwezi Ogasti 2009, ikaja kwenye nafasi ya 99 mwezi wa Septemba baada ya kupoteza alama 30, kwenye mwezi wa October.


Kichwa hichi cha mwenda wazimu kikapoteza tena alama 37 na kushuka hadi nafasi ya 106 ikiwa ni wastani wa kuporomoka nafasi 7, vibonde hawa hawakuishia hapo tu, kwenye mwezi wa Disemba ndipo walipopoteza alama 24 zilizowafanya washuke kwa nafasi 2 hadi kwenye nafasi ya 108 nafasi ambayo bado wnaishikilia tena mwezi huu wa Machi.Kwa kuangalia Orodha zaidi ya msimamo huu wa FIFA bonyeza HAPA

No comments:

Post a Comment