Sunday, March 14, 2010

ASHTON AIOMBA ISRAEL IREJELEE MAZUNGUMZO
Jumuiya ya Ulaya imetoa mwito kwa Israel ianzishe tena mazungumzo ya amani na Wapalestina.

Mwito huo unajiri kabla ya mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya, Catherine Ashton kuanza ziara ya kwanza katika Mashariki ya Kati.

Akizungumza nchini Finland, Ashton alionya kwamba juhudi za upatanishi zinaweza kusambaratika kabisa wakati ambapo aliikosoa Israel na mipango yake ya kujenga makaazi mapya ya walowezi wa Kiyahudi mashariki mwa Jerusalem.

Ashton alimtaka waziri mkuu Benjamin Netanyahu kuonyesha uongozi bora.

Alisema umaarufu wa Netanyahu nchini Israel unampa nafasi nzuri kuendeleza mazungumzo na kutafuta kile alichokitaja kama suluhisho la kudumu na maendeleo.

Mkuu huyo wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya anaanza ziara ya siku tano ya Mashariki ya Kati hii leo kwa kuanzia nchini Misiri.

No comments:

Post a Comment