Wednesday, March 3, 2010

AGATHE HABYARIMANA AACHIWA KWA DHAMANA

Mjane wa rais wa zamani wa Rwanda, hayati Juvenal Habyarimana, Agathe Habyarimana, aliyekamatwa jana na polisi nchini Ufaransa ameachiwa kwa dhamana.

Bibi Habyarimana amekuwa akitafutwa na nchi yake akiwa miongoni mwa watu wanaotuhumiwa kupanga mauaji ya halaiki ya Rwanda, mwaka 1994. Serikali ya Rwanda inamtuhumu mjane huyo mwenye umri wa miaka 68 kwa kuwa mwanachama wa kundi la Wahutu, lililopanga mauaji ya Watutsi.

Hata hivyo bado haijafahamika kama Bibi Habyarimana ambaye amekuwa akiishi nchini Ufaransa kwa miaka 12 iliyopita, atarejeshwa nchini Rwanda kwa ajili ya kusikiliza mashitaka yake.

No comments:

Post a Comment