Thursday, March 4, 2010

TAARIFA KUHUSU KAZI YA UMEME INAVYO ENDELEA ZANZIBAR





UKAMILISHAJI WA UWEKWAJI WA SEAL ZA MAFUTA NA KUFUNIKWA KWA SEHEMU ILIYOUNGWA...TRANSITION JOINT KUTOKA OIL SUBMARINE CABLE YA ZAMANI KUELEKEA XPLECONNECTION MPYA.

KAZI HIZI ZOTE ZIMEFANYIKA KWA UTULIVU NA HARAKA YA KUREJESHA NYUMA LOST TIME ZILE SIKU "ZILIZOPOTEZWA" KUTOWASILISWA VIFAA KUTOKA ERICSSON NA UK,KUTOKANA NA HALI CHAFU YA WEATHER HAPO MWEZI ULIOPITA BARANI ULAYA.

GROUP ITAYOFUATA ITAJIELEZA KUHUSU VIFAA VYA ZAMANI VIS A VIS VILIVYOWEKWA SASA NA MATARAJIO YA UBORA WAKE.

BINAFSI NATOA HONGERA WA SERIKALI CHINI YA RAIS KARUME NA WAZIRI WA WIZARA (M.U.N.A) CHINI YA WAZIRI MANSOUR NA TIMU YA ZECO CHINI YA MWENYEKITI WA BODI NDUGU MOHAMMED HASHIM NA MENEJA MKUU ZECO HASSAN ALLY NA TIMU YAKE YA ZECO WAKISHIRIKIANA NA MABINGWA WOTE WA TIMU TOKA NCHI MBALI MBALI ZAULIMWENGU.

NILIOWATAJA HAPO JUU NACHUKUA USHAHIDI WA DUNIANI NA AKHERAJINSI WALIVYOHAMISHIA OFISI ZAO NA NYUMBA ZAO HAPO FUMBA USIKU NA MCHANAHUKU MITANDAONI NA KWENGINEKO WAKILAUMIWA KWA MAKOSA AMBAYO KWA KWELI HAYASEMEKI......NDIO UKUBWA NA KISWAHILI, HAWA NDIO JAA LETU.

DHL TANZANIA INASTAHIKI PONGEZI JUU YA PONGEZI KWA KUSAFIRISHA TANI ZISIZOPUNGUA 100 KWA MADEGE AINA MBALI MBALI TOKEA PEMBE MBALI MBALI ZA ULIMWENGU.

MFANO MMOJA NI KUSAFIRISHWA TOKEA UK MAPIPA 22 YA OIL KWA EMIRATES VIA DUBAI KWA FLAT ONE DAY OUT OF HEATHROW HADI KIROMONI NA KESHOKUTWA YAKE MENGINE 12!!!! BADO TUNAYASUBIRI YALIOSAFIRISHWA KWA MELI NA WAZUNGU!!!! HUU ULIKUWA UAMUZI WA BUSARA WA SMZ NA WAZIRI KUTOJALI GHARAMA MBELE YA HUDUMA KWA NCHI YETU.

SIJAWAHI KUONA MSUKO SUKO ULIOAMULIWA KI BINGWA NA BUSARA KAMA HUU,KWA TAARIFA YA UHAKIKA UMEME ULIKUWA UREJEE MWISHO WA MWAKA KAMA PANGELIFUATWA PROCEDURE ZA KAWAIDA.

HONGERENI SANA SANA NA INSHAALLAH UREJEE UMEME WETU JUMAANNE AU KABLA NATUYASAHAU YALIOPITA TUENDELEE KUIJENGA NCHI

Eddy Riamy

No comments:

Post a Comment