Monday, February 8, 2010

WASOMALI WAWAOKOA WAHAMIAJI

Takriban watu 126 wameokolewa na wavuvi wa kisomali kutoka ghuba ya Aden baada ya wafanyabiashara wanaouza watu walipowalazimisha kuingia baharaini huku wakiwa wamewaelekezea bunduki.

Wahamiaji, wengi kutoka Somalia na Ethiopia, wamesema walitokea kaskazini mwa Somalia wiki moja iliyopita.

Wamesema boti yao ilipata hitilafu katika injini na kuelea kwa siku kadhaa kabla ya watu hao wanaouza binadamu kuanza kuwalazimisha kuingia baharini.

Watu sita mpaka sasa hawajulikani walipo.

Mwandishi wa BBC Peter Greste amesema matukio kama haya si aghlabu kutokea.

Mlinzi wa pwani katika eneo lililojitenga la Somaliland aliwagundua watu watano wa awali walionusurika wakielea kwenye maji siku ya Jumapili.

No comments:

Post a Comment