Tuesday, February 23, 2010

TUSOME UJUMBE PALE PALE TUNAPO UPOKEA

Mgonjwa mmoja mahututi alikuwa hawezi kuongea na kuwekewa oxygen akawa anaombewa na mchungaji akiwa anaombewa, yule mgonjwa akachukua kalamu na karatasi.

Akaandika na akampa yule Mchungaji, ambaye badala ya kuisoma ile karatasi, akaitia kwenye
mfuko wa joho na kuendelea na maombi hadi yule mgonjwa, AKAKATA ROHO.

Mchungaji hakuisoma ile karatasi akijua kua ni wosia wa marehemua, akasubiri baada ya mazishi kwenye kikao cha ndugu akasema:-

"KUNA KITU NILIPEWA NA MAREHEMU SIKU NILIYOKUA NAMUOMBEA"

Akampa mmoja wa wanandugu akisome, haya ndiyo yaliyokuwa yameandikwa na yule mgonjwa:

"UMEKANYAGA WAYA WA OXYGEN, NAKOSA HEWA"

JE KAMA NI NDUGU YAKO ALIEFARIKI UTAFANYA NINI ? AU UTASHAURI NINI ?

No comments:

Post a Comment