Tuesday, February 2, 2010

MAPACHA WA KISOMALI WAZUILIWA HOSPITALI

Mapacha walioungana ambao wazazi wao ni wakimbizi wa kisomali nchini Kenya wameshikiliwa katika hospitali ya Nairobi kwa miezi 16 baada ya kushindwa kulipia huduma za uzazi.
Mama wa mapacha hao wa kike, Anab Fahah Hussein, amemwambia mwandishi wa BBC kwamba familia yake inadaiwa zaidi ya dola za kimarekani elfu 30, na hospitali ya Kenyatta huku deni hilo likiongezeka kila leo.

Kundi la wasomali waishio Kenya wameanza kupokea michango ili kuwasaidia mapacha hao waweze kuondoka hospitalini.

Hospitali moja Marekani tayari imekubali kujaribu kuwatenganisha, lakini hawatoruhisiwa kusafiri mpaka walipe deni lao.

No comments:

Post a Comment