Wednesday, February 3, 2010

MTOTO WA MIAKA 13 AONEKANA KAMA NI KIZEE WA 50+

Zara Hartshorn ni mtoto mwenye umri wa miaka 13 anaeishi Rotherham Nchini Uningereza, lakini kutokana na ugonjwa wa ngozi alionao ambao kitaalamu unajuilikana kama lipodystrophy umemfanya mtoto Zara aonekane kama ni bibi wa miaka zaidi ya 50.

Mtoto huyo amekua akipata shida wakati wa kupanda mabasi, kwani pindi anapotaka kukata tiketi ya mtoto madereva humkatalia kata kata na kumtaka akate tiketi ya mtu mzima na kumwambia kua yeye si mtoto.

Skuli pia imebidi asitishe kwenda kutokana na kukosa raha, kwani wanafunzi wenzake wamembadilisha jina na kumwita jina la utani "Bibi".

Ugonjwa alionao Zara ameurithi kutoka kwa mama yake bibi Tracey Pollard, bibi huyo kwa sasa ana umri wa miaka 40 lakini anaonekana kama ni bibi wa zaidi ya miaka 70 kutokana na ugonjwa huo wa lipodystrophy.

Lipodystrophy imewahi kuwatokea watu wapatao 2,000 duniani kote na hauna tiba, hivyo Zara ataendelea kusumbuliwa na ugonjwa huo kwa maisha yake yote sawa na mama yake.

No comments:

Post a Comment