Monday, February 22, 2010

MAMA NA MTOTO WAKE WAULIWA PEMBA

Mtu mmoja Mwajuma Sahare Amour (25) na kitoto chake kichanga cha miezi (6) wameuwawa kikatili juzi usiku baada ya mama huyo kukakwa katwa na visu katika sehemu tisa katika mwili wake.

Mama huyo alipata mkasa huo baada ya mwanamme mmoja anaedaiwa kuwa alikuwa ni Mpenzi wake aliyetambulika kwa jina la Fadhili Yussuf (25) mkaazi wa Ndooni – Fundo mkoa wa kaskazini Pemba kumkata marehemu huyo katika sehemu ya tumbo ambapo alama sita zote zilikuwa katika tumbo leke na sehemu nyengine za mapajani na mkononi.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka kwa Sheha wa Shehia ya Fundo, Khamis Abeid zinasema kuwa mkasa huo ulitokea siku ya tarehe juzi majira ya saa 5.30 mchana, kijijini hapo baada ya wapenzi hao ambao walikuwa wakiishi kama mke na mume baada ya kutokea ugomvi wa kugombania mtoto

Marehemu ni Mwajume ni mzaliwa wa Kisiwa cha Fundo hapo hapo kisiwani Pemba na mtuhumiwa wa mauaji hayo Yussuf ni mzaliwa mkoa mmoja kutoka Tanzania bara.

Katika mkasa huo pamoja na kumkata mpenzi wake kwa kisu na kumsababishia Mwajuma kutokwa na damu nyingi mwilini mwake na hatimae kupoteza maisha pia aliamuwa kukinyonga kichanga hicho ambaco nacho kilipoteza maisha hapo hapo.

Kamanda wa polisi mkoa wa kaskazini Pemba Yahya Bugi hajapatikana kuthibitisha vifo hivyo vya mama na mtoto baada ya simu yake ya kiganjani kuita bila ya kupokewa.

Baada ya tukio hilo ambalo ni kubwa kufanyika kisiwani Pemba, Mtuhumiwa huyo Fadhil Yussuf, alinusurika kufa baada ya wananchi wenye hasira kutaka kumuuwa nay eye baada ya kutoka nje alipata kipigo kikubwa kutoka kwa majirani wa nyumba hiyo iliyotokea mauaji hayo ambayo yalianzia na ugomvi.

Mtuhumiwa huyo alilazimika kukimbizwa haraka katika hospitali ya Wete baada ya watu wenye hasira kumvamia na kumpiga ambapo hivi sasa amelazwa na kupatiwa matibabu huku akikabiliwa na kesi ya kuuwa kwa makusudi iwapo atatoka hospitalini hapo.

Hili ni tukio la kwanza kutokea katika Kisiwa cha Pemba la kuuliwa mama na mtoto wake pamoja kutokana na magomvi ingawaje mauwaji ya kuwania mpenzi yameshatokea mara kadhaa ksiwani hapo.

No comments:

Post a Comment