Monday, February 15, 2010

JAMBAZI AUAWA BAADA YA KUPIGWA RUNGU NA MMASAI

Mtu mmoja aliuawa baada ya kupigwa rungu la kichwa na mmasai wakati majambazi walipovamia hoteli moja ya kitalii iliopo Uroa Zanzibar.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa kusini Unguja Augustino Ollomi tukio hilo lilitokea katika hoteli ya kitalii ya Samaki Lodge ambapo watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi kuvamia hoteli hio mara tu baada ya hoteli hio kufungwa, na wageni wote kuingia vyumbani mwao kwa kulala.

Majambazi hao walivunja mlango mkubwa wa hoteli hio na kumvamia mmiliki wa hoteli hio aliyejuilikana kwa jina Fabian ambae ni raia wa Itali.

Mmiliki huyo wa hoteli alipambana na majambazi hao kabla ya kupata msaada kutoka kwa polisi ambao waliokua wakifanya doria katika maeneo hayo.

Kamanda Ollomi alimtaja aliyefaki katika tukio hilo kua ni Hassan Mohammed Abdallah mwenye umri wa miaka 44 ambae alifariki baada ya kupigwa rungu la kichwa na mlinzi wa kimasai wakati jambazi huyo alipotaka kumnyang'anya silaha askari koplo ambae alitajwa kwa ina la Mohammed.

Katika tukio hilo pia askari wawili pamoja na jambazi mmoja walijeruhiwa, askari waliojeruhiwa ni pamoja na koplo Mohammed Salum ambae amejeruhiwa sehemu za kichwa na shingo pamoja na kamanda wa polisi wilaya ya kati ASP Juma Said ambae alijeruhiwa mkononi baada ya kuchinjwa kwa kiwembe na mmoja wa majambazi hao.

Polisi walifanikiwa kumkamata Abdallah Juma Faki mwenye umeri wa miaka 45 mkaazi wa Mwembe Makumbi ambae alijeruhiwa baada ya kupigwa na wananchi wenye hasira na kulazwa katika hospitali ya Mnazi Mmoja.

No comments:

Post a Comment