Sunday, February 7, 2010

DROGBA AWALIZA ARSENAL

Magoli mawili yaliyopachikwa na mshambuliaji machachari wa Chelsea Drogba leo hii walipocheza dhidi ya washika bunduki Arsenal imewarudisha tena Chelsea kileleni mwa ligi kuu ya Uingereza, mechi hio iliyochezwa katika uwanja wa Stamford Bridge ulikua ni wa upande mmoja ambapo Chelsea waliutawala sana mchezo na washika bunduki kuonekana si lolote si chocho huku wakicheza pasi zao fupi fupi zisizo na mafanikio, kwa matoke hayo Chelsea wanaongoza msimamo wakiwa na alama 58 ikiwa ni tofauti ya alama mbili tu MANU ambao wako nafasi ya kwa alama 56 na nafasi ya tatu wapo washika bunduki na alama zao 49.

No comments:

Post a Comment