Thursday, February 11, 2010

BABU SEYA NA PAPII KOCHA WARUDISHWA TENA JELA

Mahakama ya rufaa leo imewarudisha tena jela Nguza Viking (Babu seya) pamoja na mwanawe Papii Nguza (papii kocha) na kuwaachia huru Nguza Mbagu na Francis Nguza.

Babu seya pamoja na wanawe watatu walihukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kupatika na makosa ya ubakaji wa watoto wadogo wenye umri wa miaka 6 hadi 8 mwaka 2003

Katika kesi iliyosikilizwa leo katika mahakama ya rufaa ambayo iliendeshwa kwa muda wa masaa matatu na kutolewa hukumu ilisababisha vilio baada ya mahakimu Nathalia Kimaro, Mbarouk Mbarouk na Salum Massati kuwaamuru Babu Seya na Papii kocha kurudi jena,kwa upande wa utetezi kesi hio ilikua ikisimamiwa na mawakili Mabere Marando and Hamidu Mbwezeleni,

No comments:

Post a Comment