Sunday, January 3, 2010

MWANAZUONI KUTOKA JAMAICA AKAMATWA NCHINI KENYA

Mwanazuoni wa kiislam kutoka Jamaica ambaye aliwahi kufukuzwa kutoka Uingereza kwa makosa ya kuchochea uhasama kwa misingi ya rangi anafanyiwa uchunguzi na polisi nchini Kenya, baada ya kukamatwa na kikosi maalum cha kupambana na ugaidi akiwa katika mji wenye bandari wa Mombasa.

Mwanazuoni huyo Sheikh Abdullah al-Faisal, alishikwa katika mkesha wa mwaka mpya kwa madai ya kukiuka kanuni za uhamiaji kwa kuhubiri katika misikiti.

Kundi la kiislam la kutetea haki za binadamu nchini Kenya lilisema kuwa liliarifiwa na serikali kuwa mwanazuoni huyo atafukuzwa nchini.

Mkuu wa kundi hilo, al-Amin Kimathi, alisema mwanazuoni huyo alialikwa na makundi ya kiislam katika miji ya Mombasa na Nairobi.

Amesema kitendho cha kumkamata kilichochewa na ubaguzi, ambapo imekuwa mazoea wanazuoni wa kiislam kutiwa kizuizini na hata kufukuzwa nchini bila sababu zinazoeleweka.

No comments:

Post a Comment