Sunday, January 3, 2010

MAPACHA WALIOUNGANA WAFARIKI DUNIA

Watoto mapacha walioungana waliozaliwa na bibi Farhat Maulid siku ya mkesha wa mwaka mpya katika hospitali ya Mnazi mmoja wamefariki dunia jana Januai 2, 2010 asubuhi katika hospitali ya taifa ya Mnazi mmoja.

Watoto hao ambao wameishi kwa siku moja tangu kuzaliwa kwao na kuhifadhiwa katika chombo maalum cha kusaidia joto (INCUBATOR) pamoja na kusaidiwa kupumua hali yao ilikua inaendelea vizuri.

Kwa mujibu wa daktari amesema watoto hao wamefariki dunia saa12 asubuhi jana 2/1/2010, baada ya kuishi kwa takriban masaa 11 tangu kuzaliwa kwao na mauti yamewakuta kabla ya kutenganishwa kwa miili yao.

Mama mzazi wa marehemu hao bibi Farhat Maulid mwenye umri wa miaka (18)ambae ni mkaazi wa Mwanyanya wilaya ya Magharibi hali yake inaendelea vizuri katika hospitali ya Mnaei mmoja.

Watoto hao walikua wameungana sehemu ya kifuani na tumboni wakiwa na uzito wa kilo 3, ambao walizaliwa kwa njia ya operesheni lilikua ni tukio la kwanza kutokea katika visiwa vya Zanzibar.

Watoto hao walikua wakitumia baadhi ya viungo kama kitovu na moyo mmoja, lakini viungo vilivyobakia kila mmoja alikua akitumia chake.

Tunamuomba Allah ampe subira na afya njema mama wa marehemu hao bibi Farhat Mauli.

Amiin.

No comments:

Post a Comment