Monday, December 7, 2009

ZANZIBAR YAINGIA NUSU FAINALI KWA NJIA YA MATUTA

Timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes imefanikiwa kuingia nusu fainali ya michuano ya Chalenji inayoendelea nchini Kenya baada ya kuitoa timu ya Zambia kwa njia ya matuta baada ya mechi hio kutoka sare kwa mabao 0-0,katika mechi hio Zanzibar ilishinda kwa penalty 4-3 huku kipa Zanzibar Mohammed akipangua penalty mbili.

Tunaipongeza sana timu hio kwa ushindi waliopata na kuwatakia kila la kheri katika mechi ya nusu fainali.Vile vile tunawatakia kila a kheri ndugu zetu Tanganyika katika mechi yao ya kesho watakapojitupa uwanjani kuminyana na Etitrea kwa kuwania tiketi ya kucheza nusu fainali.

No comments:

Post a Comment