Sunday, December 6, 2009

KEVIN ARAMBA $200,000 BIG BROTHER REVOLUTION 2009

Hatimae mnigeria Kevin amenyakua kiticha cha $200,000 baada ya kuibuka mshindi katika shindano la Big Brother Revolutin 2009 huko Afrika Kusini, shindani hilo lilimalizika leo hii baada ya watu watano waliokua wamebakia ndani ya nyumba hio kutolewa mmoja baada ya mmoja.

Ilikua ni pale IK alipoaanza kwa kumtaja Nkema kutoka Nigeria kwa ajili ya kutoka kwenye jumba hilo ambae ameshika nafasi ya tano,huku akifuatiwa na Mzamo mwenye miaka 24 kutoka Malawi nae alishika nafasi ya nne.

IK baadae aliendelea kwa kumtaja Edward Mnamibia mwenye umri wa miaka 33 ambe alikua hasimu mkubwa wa Kevin pamoja na Mtanzania Elizabeth.

Mwisho walibaki washiriki wawili Emma na Kevin, ndipo IK alipolazimika kumtaja mshindi wa shindano hilo, na kumtaja Kevin.

Kevin alishindwa kuzuia machozi baada ya jina lake kutajwa kua ndie mshini wa shindano hilo,na hivo kujinyakulia kitita cha dola za kimarekani $200,000.

Wasihiriki wote waliotolewa nao pia hawakuondoka mikono mitupu,walibahatika pia kuondoka na kifutia jasho.

No comments:

Post a Comment