Friday, December 18, 2009

WASOMALI WAACHIWA BAADA YA KUKOSA SEHEMU YA KUSHITAKIWA

Kundi la watu wanaoshukiwa kuwa maharamia wa kisomali waliotiwa kizuizini katika meli ya kivita ya Denmark wameachiliwa huru.
Washukiwa hao wameachiwa kwasababu hakuna nchi yeyote iliyokubali kuwafungulia mashitaka.

Taarifa iliyotolewa na wizara ya ulinzi ya Denmark imesema Umoja wa Ulaya uliamua kwamba washukiwa hao 13 walitakiwa kuachiwa huru kutokana na ugumu wa kuwafungulia mashitaka.

Washukiwa hao walikamatwa katika bahari ya Hindi wiki mbili zilizopita baada ya kudaiwa kufanya jaribio la kushambulia meli ya mizigo.

Walirejeshwa kwenye boti yao wenyewe wakisaidiwa na chakula pamoja na mafuta.

No comments:

Post a Comment