Thursday, December 10, 2009

KUONDOKA KWA ETO' O BARCA NI KUPOROMOKA KWA KIWANGO AMA NI CHUKI ZA GUARDIOLA

Eto’o alimaliza msimu wa 2008-2009 huko Hispania akiwa amefunga magoli 30 katika mechi 36 za ligi, pamoja na magoli mengine sita katika mechi 12 za Ulaya wakati Barcelona iliposhinda vikombe viwili La Liga na Ligi ya vilabu bingwa barania Ulaya.
Hayo yote yalitokea licha ya kocha mpya wa Barca, Pep Guardiola kusema hadharani kuwa hakuwa akimhitaji tena mchezaji huyo wa kimataifa wa Cameroon.

Lakini Eto’o alimaliza msimu kwa kishindo, alifunga goli la kwanza katika ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Manchester United kwenye mechi ya fainali ya ligi ya vilabu bingwa Ulaya mjini Rome.

Goli hilo lilimfanya Eto’o kuwa mchezaji wa pili kati ya wawili – mwingine Raul wa Hispania kuweza kufunga katika fainali za kombe la vilabu bingwa Ulaya. Eto’o pia alifunga goli wakati Barca ilipoifunga Arsenal kwenye fainali za mwaka 2006.

Hata hivyo Barca hawakutaka kumbakisha mwanasoka huyo ambae keshachukua taji la mwanasoka bora wa Afrika mara tatu, aliishia kupelekwa kwa mabingwa wa Italia, Inter Milan kama sehemu ya mpango wa kumpata Zlatan Ibrahimovic.

Mshambuliaji huyo mwenye uchu wa magoli alianza vizuri maisha yake mapya ya Italia katika ligi ya Serie A, akiwa na timu yake mpya ya Inter, hadi mwisho wa mwezi wa Novemba alikwishafunga magoli sita katika mechi za ligi ambayo maisha ya washambuliaji huwa magumu.

Eto'o alitangazwa rasmin kuwa nahodha wa timu ya taifa ya Cameroon na kocha wa kifaransa Paul Le Guen na mara baada ya kutangazwa kuwa nahodha mwezi Agosti, Cameroon ilijikwamua na kuziba pengo la pointi mbili katika kundi A na hatimaye kuongoza katika kipindi kifupi.

Huko Indomitable Lions wakidhihirisha umwamba wao kwa kushinda mechi nne muhimu, Eto'o mwenye umri wa miaka 28 alifunga magoli manne wakati timu yake ilipofuzu ikiwa na pointi nne mbele ya timu inayofuatia.

Kwa Barcelona na Cameroon mwaka 2009, Samuel Eto’o alikuwa hashikiki.

No comments:

Post a Comment