Wednesday, November 11, 2009

TUNAFAHAMU NINI KUHUSU MAENDELEO?

Katika kufuatilia kwangu habri katika mambo ya maendeleo ya nchi ya Tanzania nimeona kua imeelezwa sana kwenye vyombo vyahabari Tanzania imepiga hatua kimaendeleo na katika ule mpangilio wa nchi ya kwanza kwa utajiri hadi kufikia nchi masikini kuliko zote duniani nimeona kwamba Tanzania imepiga hatua, ila nimesahahu tu imeshika nambari ya ngapi.

Lakini mimi hua najiuliza kila siku hivi haya maendeleo yaliopatikana hadi kuipandisha chati Tanzania ni kwa kigezo gani? kwa sababu kwa kua mimi sio msomi na wala sio mwana uchumi ninavojua mimi tunaposemna neno maendeleo katika nchi hapa ina maana kwanza nchi ifikie jambo ambalo halikuwepo kabla hususan katika mambo ya kijamii yawe yamepiga hatua kwa mfano katika elimu, afya, maji safi umeme, n.k.

lakini tangu nianze kupata fahamu yangu nasikia Tanzania ina tatizo la umeme, na naweza kusema kwamba tangu mimi sijazaliwa inajuilikana kama tatizo la ukosekanaji wa umeme linasababishwa na kitu gani lakini hadi hivi ninavyoandika habari hizi ni zaidi ya miaka 40 kuna tatizo la umeme au haya ndio maendeleo

Katika suala la elimu hali ndio hio hio, kwa sabau mimi nakumbuka siku hizo nilipokua nasoma tulikua tukipewa vifaa vyote vya kusomea kama vitabu, mabuku, peni , penseli, n.k bure, na hakuna hata mwanafunzi mmoja katika skuli hata moja aliekua akikaa chini, lakini katika nchi hio hio iliopiga hatua katika maendeleo wanafunzi wanakaa chini na hawapewi hata penseli, kila kitu unapaswa ujinunulie mweyewe,hali kadhalika hivo ndivyo ilivo katika kila jambo linalohusu jamii.

Ukiangalia kila siku nchi hii inazungumza huyu kaiba bilioni mia ngapi na huyu kaiba bilioni mia ngapi wanaita ufisadi sasa je hakuna mambo ya kushughulikia zaidi ya huu ufisadi usiokwisha? au hizi ni njama maalum zilizotengezwa ili kuzubaisha watu akili? kwa sababu kama huu ufisadi mbona hakuna hata mmoja aliehukumiwa? mbona viongozi hawafatilii mambo muhimu ya kijamii wameshika tu ufisadi ufisadi ufisadi, au maendeleo yenyewe ndio haya ya kutueleza mambo ya ufisadi kila siku na hizi kelele za kumuenzi Nyere zisizokwisha?

Maendeleo haya yanayozungumzwa yamepatikana katika kitu gani? au ni yale majumba makubwa yanayojengwa katika mji wa Dar-es Salaam? mimi sijui, naomba wataalamu wa mambo ya uchumi wanifahamishe.

Mzanzibari halisi.

1 comment:

  1. hapa kwa kweli mimi najiuliza kila siku ni maendeleo gani hayo ambayo tanzania imepiga hatua? hakuna umeme maji hakuna wanafunzi wanakaa chini chakula hakinunuliki ilimradi balaa tu

    ReplyDelete