Friday, November 6, 2009
SIEF SHARIF AKUTANA NA AMANI KARUME
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Amani Abeid Karume leo amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Chama cha CUF, Maalim Seif Sharif Hamad huko Ikulu, Mjini Zanzibar.Katika mazungumzo hayo, ambayo hayakutarajiwa na wengi wawili hao yaligusia mambo mbali mbali ikiwa ni pamoja na haja ya kudumisha amani na utulivu nchini na maelewano na mashirikiano kati ya wananchi wote.
Viongozi hao wamezingatia haja ya kuzika tofauti zilizopo ambazo zinachangia kuwatenganisha Wazanzibari na kutoa wito kwa viongozi wa vyama vyote vya siasa na wananchi kwa jumla kushirikiana katika kujenga nchi bila ya kujali itikadi zao za kisiasa.
Viongozi hao walifafanua kuwa wananchi wakishirikiana na kujenga nchi kwa pamoja, watapiga hatua kubwa zaidi za maendeleo.Katika mazungumzo hayo, viongozi hao walihusisha umuhimu wa mchakato wa mazungumzo endelevu baina yao na vyama vyao kwa jumla.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment