Wednesday, November 25, 2009

PICHA YAMDHALILISHA MICHELLE OBAMA

Kampuni ya Google imeomba msamaha kutoka kwa Michelle Obama, mkewe rais wa Marekani kutokana na picha inayomdhalilisha na ambayo imechapishwa kwenye mtandao.
Picha yenyewe imechorwa kwa mfano wa mnyama na inajitokeza pindi mtu anapotafuta kwenye mtandao picha zozote za Michelle Obama.

Google imeomba radhi na kukiri kwamba picha hiyo ambayo tayari imezua hoja kali inachochea hisia za ubaguzi wa rangi.

Kampuni hiyo imetoa tahadhari kwa wale wanaotembelea mtandao na kutafuta picha za Michelle Obama ingawa ilisema haiwezi kuiondoa hiyo picha.

Ikulu ya Marekani, White House, imekataa kutamka lolote kuhusu tukio hilo.

No comments:

Post a Comment