Monday, November 16, 2009

NGUVU YA HoH KISHERIA YAMUOKOA ITAI BBA

Mambo yamezidi kupamba moto ndani ya jumba la Big Brother wiki hii baada ya majina mawili kutajwa kwa ajili ya kufukuwa siku ya jumapili ijayo, majina yaliyotajwa ni Emma pamoja na Itai

Wakati huo huo Itai yeye mwenyewe amechaguliwa kuwa mkuu wa nyumba kwa wiki hii( HoH),kisheria mkuu wa nyumba anakua na fursa ya kumuokoa mtu mmoja ambae yuko juu na ambadilishe na mwengine, kwa hio Itai alipotakiwa kufanya hivo na Big Brother ndipo alipopata nafasi ya kujiokoa yeye mwenye na kujibadilisha na Geradine kwa hio waliokua juu wiki hii ni Emma na Geradine

Kwa hio tunasubiri siku ya jumapili ili kuangalia kama je Emma atanusurika kwa mara nyengine tena? kwa sababu aliwahi kunusurika siku za nyuma.

No comments:

Post a Comment