Monday, November 16, 2009

KOFIA ZA KIUA NDANI YA ZANZIBAR

Kuna rafiki yangu mmoja amenitumia hii picha na ameniambia niulize kama je kuna sehemu yoyote ambayo kuna wataamu wa kushona kofia za kiua kuliko Makunduchi Zanzibar?
maana anasema kila mmakunduchi anajua kushona hizi kofia.

sasa mimi sijui kama ni kweli au anajisifu tu kwa hio kama kuna mwenye hoja ataniandikia

4 comments:

 1. Ni kweli mmakunduchi yeyote au alieshi utotoni kwakwe mpaka akawa na fahamu zake ,ushoni wa kofia ya kiua ataijua tu, mie nimejifunza huko

  ReplyDelete
 2. sasa na mimi ningeomba niulize, kwa nini kofia ya kiua mshonaji mwengine na muunganishaji ule mshazari na ile sehemu nyengine (nimeisahau jina) anakua mwengine? kwa sababu nahisi ile kazi ya kushona vile viua ndio ngumu kuliko kuiunganisha ile kofia.

  ReplyDelete
 3. Hilo liko wazi ,kwani gari inakamilika kwa mtu moja si kila kitengo kinafanya vyake.

  Nirudi kwenye kofia washiriki ni wanne:
  1.mtengenezaji mshazari.
  2.mshoma kofia( atia viua)
  3.muungaji mshazari baadae ya viua
  4.Muuzaji 1 ( kofia fresh kutoka 2)
  5.Dalali muuzaji 2 ( hapo mezani -darajani n.k)

  ReplyDelete
 4. Kwa hali hii lazima kiuwa kiuzwe bei ghali

  ReplyDelete