Saturday, October 10, 2009

ENGLAND YASHINDWA KUWEKA REKODI

Ndoto za England kufuzu kucheza final za kombe la dunia 2010 huko Afrika Kusini bila ya kufungwa mechi hata moja leo zimegonga mwamba baada ya kufungwa katika mechi yao ya 9 bao moja na Ukraine mechi ambayo ilichezwa katika uwanja wa Dnipro Stadium Ukraine.Ukraine walifunga goli hilo kwa njia ya tuta baada ya Rober Green kumchezea rafu Artem Milevskiy ndani ya box na kutolewa nje kwa kadi nyekundu.England walimtoa winga wao machachari Aaron Lenon ili kumuwezesha David James kuingia,kwa mtokeo haya Ukraine imejipa matumaini ya kufuzu baada ya kujivuta katika nafasi ya pili wakiwa na alama 18 lakini watalazimika kushinda katika mechi yao ya mwisho watakapocheza siku ya jumatano tarehe 14 octoba dhidi ya Andora katika uwanja wa Estadio Comunal la Vella, Andora.

No comments:

Post a Comment