Saturday, October 24, 2009

MWANAMKE APATWA NA UGONJWA BAADA YA KUDUNGWA SHINDANO YA KINGA YA MAFUA YA NGURUWE

Desiree Jennings, 25, alipatwa na ugonjwa unaompata mtu mmoja kati ya watu milioni moja baada ya kuchomwa sindano ya kinga ya mafua ya nguruwe ambayo ilisababisha awe kama amepooza.

Jennings hupatwa na maumivu makali sana anapotembea kwenda mbele na hulazimika kujinyonga nyonga na kuzungusha miguu yake ili kupunguza maumivu hayo lakini hata hivyo hawezi kutembea umbali mrefu.

Lakini hali hiyo hutoweka kabisa na hutembea vizuri kabisa anapotembea kinyume kinyume.

Cha ajabu zaidi huweza kukimbia kwenda mbele bila ya matatizo yoyote lakini anaposimama hali hubadilika na huhitaji mtu kumsaidia asianguke.

Hali hiyo ilimtokea siku 10 baada ya kuchomwa sindano hiyo ya kinga ya ugonjwa wa mafua ya nguruwe H1N1.

Ndoto ya Jennings kuwa mcheza shoo ya ushangiliaji wa timu ya soka ya Marekani ya Washington Redskins imetoweka baada ya kukumbwa na hali hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na madaktari Jennings anasumbuliwa na ugonjwa unaowapata watu wachache sana duniani unaoitwa dystonia.Ugonjwa huo huifanya misuli isinyae na kupelekea hali hiyo aliyo nayo.

Chini ni video yake inayomuonyesha jinsi anavyotembea kwa tabu kwenda mbele huku akitembea kinyume nyume bila matatizo yoyote.

No comments:

Post a Comment