Monday, September 28, 2009

WANAFUNZI SKULI YA KIBASILA WAANDAMANA NA KUFUNGA NJIA YA CHANG'OMBE NA MANDELA ROAD

Wahusika katika jeshi la polisi walifika eneo la tukio na kujadiliana juu ya nini cha kufanya


Jinsi walivokua wamekaa barabarani hapo kama vile hakuna jambo lolote linaloendelea


waliamua kuimba na kucheza barabarani hapo



Wanafunzi katika shule ya kibasila mijini Dar-es-salaam waliandamana leo mchana na kufunga barabara ya chang'ombe na Mandela road kufuatia ajali za mara kwa mara kwa wanafunzi katika eneo hilo.
Wanafunzi hao wamenzisha maandamo hayo ambayo hayakua na kibali kutoka kwa wakuu wa skuli, jeshi la polisi wala kutoka kwa mkuu wa wilaya.
Wanafunzi hao walidai kwamba hawataondoka sehemu hio hadi pale wahusika wakuu watakapo kuja na kuzungumza nao ili kutoa tamko rasmi la kuwekewa alama za barabarani katika eneo hilo, barabara hio haina alama yeyote ya na hivo kusababisha vifo vya kila siku kwa wanafunzi wa skuli hio.





No comments:

Post a Comment