Wednesday, July 21, 2010

SAMAKI WA NDUARO WALIEVULIWA NUNGWI

Wachukuzi wa samaki katika marikiti kuu ya samaki darajani wakimshusha samaki aina ya nduaro aliyevuliwa kijiji cha nungwi ambaye ameuzwa shillingi 1,500,000 katika soko la Nungwi.
Mchuuzi wa samaki marikiti kuu Darajani akimkata mapande samaki aina ya nduaro kwa ajili ya kuuzwa sokoni hapo samaki huyu anakadiriwa kufika zaidi ya tani mbili.

Wadau mlio ughaibuni mmeona hygiene - jinsi tunavyohakikisha hatupatwi na vijidudu vinavyosababisha maradhi licha ya Nduaro kushughulikiwa chini ambako hali yake ya usafi kama unayoiona. Kwani hata pweza kwanza lazime apate kichapo cha kupigwa na chini ili aregee na chini kwenyewe ni sehemu yoyote. Kisha huoshwa tayari kwa mapishi. Othman Mapara

No comments:

Post a Comment